Duration 1:3:22

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA MORNING GLORY THE SCHOOL OF HEALING 29/ 11 / 2021

6 624 watched
0
140
Published 29 Nov 2021

KKKT USHARIKA WA KIJITONYAMA : IBADA YA MORNING GLORY THE SCHOOL OF HEALING MAFUNGO YA SIKU AROBAINI MADA: TABASAMU TENA- SMILE AGAIN MAWAZO YA KUFIKIRIKA "Let your SMILE change the world, Don't let the world change your SMILE" (Ruhusu TABASAMU lako libadilishe Ulimwengu; wala usiruhusu ulimwengu ubadilishe TABASAMU lako) UJUMBE WA LEO : 29/11/2021 MKUKI WA SAULI NA RIZIKI YANGU Luka 11 : 1 - 4 1 Ikawa alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake. 2 Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. 3 Utupe siku kwa siku riziki yetu. 4 Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni lakini tuokoe na yule mwovu. 1 Samweli 18 : 6 - 9, 11 - 12 6 Hata ikawa, walipokuwa wakienda, hapo Daudi aliporudi baada ya kumwua yule Mfilisti, wanawake wakatoka katika miji yote ya Israeli, kwa kuimba na kucheza, ili kumlaki mfalme Sauli; wakatoka na matari, na shangwe, na vinanda. 7 Nao wale wanawake wakaitikiana wakicheza, wakasema, Sauli amewaua elfu zake, Na Daudi makumi elfu yake. 8 Basi Sauli akaghadhibika sana, na maneno haya yakamchukiza; akasema, Wamempa Daudi makumi elfu, na mimi wamenipa elfu tu; kuna nini tena awezayo kupata, isipokuwa ni ufalme? 9 Sauli akamwonea Daudi wivu tangu siku ile. 11 Mara Sauli akautupa ule mkuki; maana alisema, Nitampiga Daudi hata ukutani. Daudi akaepa, akatoka mbele yake, mara mbili. 12 Sauli akamwogopa Daudi, kwa sababu Bwana alikuwa pamoja naye, ila amemwacha Sauli. 1 Samweli 2 : 6 - 9 6 Bwana huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. 7 Bwana hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. 8 Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina Bwana, Naye ameuweka ulimwengu juu yake. 9 Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda; Ezekieli 5 : 16 16 hapo nitakapopeleka mishale mibaya ya njaa juu yao, iletayo uharibifu, nitakayoipeleka ili kuwaharibu ninyi; nami nitaiongeza njaa juu yenu, na tegemeo lenu la mkate nitalivunja. Mhubiri : Mwl Emilian Katubayemo Kwa maombi na ushauri: Mch. Dkt. Eliona Kimaro. Simu :+255655516053, +255754516053 YouTube : Rev. Dr. Eliona Kimaro TV Barua Pepe: elionakimaro555@gmail.com

Category

Show more

Comments - 41