Duration 2:24

ONGEZEKO LA MAJI ZIWA TANGANYIKA LAATHIRI BIASHARA YA SAMAKI, SERIKALI KUJENGA SOKO JIPYA KASANGA

42 watched
0
0
Published 10 May 2021

Serikali imesema katika kipindi cha muda mfupi ujao inatafuta eneo kwa ajili ya kuweka mwalo na soko la muda la kuuzia samaki katika Kata ya Kasanga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa, kufuatia mwalo na lililokuwa soko la kata hiyo kujaa maji baada ya kina cha maji cha Ziwa Tanganyika kuongezeka. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah amesema hayo mwishoni mwa wiki baada ya kutembelea eneo hilo na kujionea uharibu mkubwa wa miundombinu ya soko na mwalo kufunikwa na maji na kubainisha kuwa wizara inatafuta eneo la muda huku ikitafakari pia mipango ya muda mrefu kujenga sehemu ambayo ni salama zaidi. USISAHAU KU SUBSCRIBE CHANNEL YETU ILI UWE UNAPATA UPDATE MPYA KILA TUNAPO WEKA HABARI MPYA WAKATI WOWOTE BONYEZA HAPA CHINI KWENYE MAANDISHI YA BLUU /channel/UCcCo ... https://www.instagram.com/kahamatvonline/ #KAHAMATVONLINE #HABARIZAHIVIPUNDE

Category

Show more

Comments - 0